Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda, amelipongeza Shirika la Mzinga kwa kuanzisha Mradi wa Kokoto Mkoa Arusha uliopo chini ya Kampuni Tanzu ya Shirika hilo.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la mradi huo uliopo eneo la Nanja Wilayani Monduli Leo tarehe 03 Mei 2025. Jenerali Mkunda amelipongeza Shirika kuanzisha Mradi wa Kokoto wa Kimkakati.
Amewataka wasimamizi wa mradi huo kuwa makini na kutanguliza maslahi ya Shirika na kuuendesha kwa faida ili uwe shamba darasa kwa miradi mingine.
Akitoa taarifa ya mradi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mzinga Luteni Jenerali Samwel Ndomba (Mstaafu) amemhakikishia Mkuu wa Majeshi kuwa Mradi huo utasimamiwa kwa umakini sana ili uwe na tija na kuchangia Uchumi wa Taifa.
Kwa upande wa Meneja Mkuu Shirika la Mzinga, ambalo linaendesha Kampuni Tanzu ya Mzinga, Brigedia Jenerali Seif Athumani Hamisi amesema Mitambo ya Mradi huo iliyofungwa ni ya kisasa na itakuwa na uwezo wa kuzalisha Kokoto Tani Mia Tatu (300) kwa saa moja.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.