Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini,Jenerali Venance Mabeyo leo Februari 15, 2021 amefanya ziara katika Vikosi vilivyopo Kanda ya Shinyanga na kuzungumza na Maafisa na Askari wa vikosi hivyo.
Akizungumza na Maafisa na Askari wa Kanda hiyo, Mkuu wa Majeshi amewapongeza kwa kuendelea kudumisha nidhamu na kufanya kazi kwa weledi ili kuliwezesha Jeshi kufikia malengo yake.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Majeshi amepata nafasi ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na vikosi vilivyopo kanda hiyo na kuwaasa waendelee kufanya kazi kwa bidii.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 9203 Dar es Salaam,
Street :Magore, Upanga
Fax : +255 22 2153432
Tel : +255 22 2150592- 4
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.