Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amefanya ziara maalum ya kikazi mkoani Rukwa, ambapo leo tarehe 21 Novemba amevitembelea vikundi vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vilivyopo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi na kujionea utayari wa vikundi hivyo katika jukumu zima la ulinzi wa mipaka ya nchi.
Hapo awali Jenerali Mabeyo alifanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mhe. Said Mohamed Mzanda ambaye pia ndie Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo.
Mhe. Mzanda alisema Hali ya Ulinzi wilayani humo mpaka sasa ni salama na kulishukuru Jeshi kwa jitihada zake katika suala zima la ulinzi wa mipaka ya nchi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.