Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo leo ameipokea timu ya Golf ya Lugalo ambayo imeshiriki Mashindano ya Wazi ya Golf kwa Wanawake nchini Nigeria na kuibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo.
Michuano hiyo ilifanyika mjini Abuja na kushirikisha mataifa kumi (10) yenye jumla ya wanamichezo zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.
Wakati huohuo Jenerali Venance Mabeyo amewapandisha cheo askari wawili washiriki kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo kutoka cheo cha Praiveti na kuwa Koplo.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.