Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo leo amekutana na Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma wanaofanya kazi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani katika kikao kilichofanyika kwenye viwanja vya Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho Mkuu wa Majeshi alitoa salam za mwaka mpya na kuwashukuru Maafisa na Askari kwa kufanya kazi kwa weledi, kwa mafanikio makubwa yaliopatikana mwaka jana na kusisitiza kuyaendeleza mafanikio hayo ili mwaka 2019 uwe wa mafanikio zaidi.
Vilevile aliwakumbusha Maafisa na Askari kuendeleza na kuudumisha ushirikiano mzuri kwa ngazi zote baina ya JWTZ na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama. Alisema mshikamano ndio dira ya kuletaupendo na kutambua majukumu ambayo tunapaswa kuyatekeleza kulingana na kiapo chetu kwa lengo la kulitumikia Taifa.
“Wajibu wa kwanza wa mwanajeshi ni kulinda mipaka ya nchi, watu pamoja na mali zao” alisema Jenerali Mabeyo. Aidha, aliwataka Maafisa na Askari kuwa wa kwanza katika kuwalinda wananchi kwani Wanajeshi ni tegemeo la wananchi kiulinzi.
Pia aliwataka Maafisa na Askari kutii na kuthamini kiapo chao na kuweka uzalendo mbele ili kuwezakufanya kazi kwa ufanisi. “Changamoto tulizozipata mwaka jana katika kutekeleza majukumu yetu tuzigeuze kuwa fursa kwa mwaka huu wa 2019” alisema Jenerali VenanceMabeyo.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.