Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),linapenda kutoa tahadhari kwa umma juu ya uwepo wa vikundi au watu wanaojifanya kuwa na uwezo wa kuwapatia vijana wa kitanzania ajira za moja kwa moja katika JWTZ au nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kujitolea.
JWTZ na JKT limekuwa likitoa ufafanuzi mara kwa mara wa namna ajira za JWTZ na nafasi za JKT zinavyopatikana.Usaili wa vijana wanaotaka kujiunga na JKT huanzia ngazi ya vijiji,kata, vijiji,wilaya hadi mkoa waliofaulu usaili na vipimo vya afya hupewa form za kujaza.
Pamoja na wananchi kusisitizwa kwamba hakuna gharama zozote zinazotozwa ili kupata nafasi hizo bado baadhi yao hutoa fedha kama ‘rushwa’ ili kupatiwa nafasi kinyume na taratibu zilizowekwa.kwa kukiuka taratibu zilizowekwa,wengi wamejikuta wakitapeliwa fedha zaobila kupata nafasi hizo.Baada ya kukosa nafasi hulazimika kumfuata kiongozi wa Jeshi ili kurejeshewa.
Nafasi za kujiunga na mafunzo ya JKT,hutolewa na Makao Makuu ya JKT kwa matangazo rasmi kupitia vyombo vya habari vilivyopo nchini na siyo kupitia mitandaoya kijamii wananchi wote wanatakiwa kuzingatia utaratibu huo.
Mwananchi yeyote atakayetoa fedha kwa namna yoyote ile ili kijana wake ajiunge na JKT na kisha kuwasilisha malalamiko kwamba ametapeliwa atahesabika kuwa ametoa ‘rushwa’ hivyo na
Yeye atafikishwa katika vyombo vya sheria kwa tuhuma za kutoa ‘rushwa’.Ikumbukwe kuwa, Mtoa Rushwa na Mpokea Rushwa wote ni wakosaji kwa mujibu wa sheria.
Wananchi wote mnatahadharishwa kuacha kutumia njia zisizo sahihi katika kutafuta ajira katika JWTZ au nafasi za kujiunga na JKT.Ni dhahili kuwa ukitoa fedha kwa utaratibu huo fedha yako itakuwa imepotea na nafasi hiyo hutapata.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.