Timu ya mpira wa kikapu ya JKT wanaume imefanikiwa kutinga nusu fainali katika mashindano ya BAMMATA yanayoendelea jijini Dodoma baada ya kuifunga timu ya Magereza wanaume kwa jumla ya vikapu 92 kwa 44.
Akizungumza mara baada ya mchezo kumalizika kocha wa timu ya JKT Christian Jackob Mwakingili amesema morali pamoja na nidhamu ya mchezo ndio imewawezesha kuibuka na ushindi huo mkubwa.Aliongeza kwa kusema "tangu awali tulitegemea kufika fainali na hatimaye kuchukua kombe hivyo tumejiandaa vya kutosha" .
Katika mchezo wa kikapu uliotangulia Ngome wanaume waliwaondoa Polisi wanaume na hivyo kutinga fainali na sasa watakutana na JKT ambao wameonesha kuwa na kiwango kizuri na kuzingatia maadili ya mchezo na hivyo kuifanya fainali hiyo kutegemewa kuwa na ushindani mkubwa kwani timu ya Ngome nayo imejiandaa vya kutosha.
Mashindano hayo ya BAMMATA kwa mwaka huu yanafanyika jijini Dodoma katika viwanja vya Shule ya St. John Merlin iliyopo maeneo ya St. Gema kwa kuzishirikisha timu mbalimbali za Vyomba vya Ulinzi nchini.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.