Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Marekani pamoja na Majeshi ya Mataifa mengine 13 wamehitimisha Zoezi la pamoja la Kijeshi la Majini "CUTLASS EXPRESS" lililolenga kuimarisha Usalama wa Majini kupitia kubadilishana Uzoefu wa kimbinu na kuboresha ujuzi wa pamoja katika kukabiliana na changamoto na Matishio ya Ulinzi na Usalama katika Bahari.
Akizungumza katika hafla ya kufunga Zoezi hilo kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Jacob John Mkunda, Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita JWTZ Meja Jenerali Ibrahim Mhona amesema lengo la Mafunzo ni namna ya kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu, madawa ya kulevya, silaha na kupambana na Uharamia.
Aidha, Meja Jenerali Mhona amesema kupitia mazoezi hayo maafisa na Askari wa JWTZ wameweza kujengewa uwezo zaidi.
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Marekani nchini Mhe. Andrew Lentz amesisitiza kuwepo na ushirikiano thabiti baina ya Mataifa hayo ili kusaidia udhibiti wa matishio mbalimbali baharini.
Zoezi hilo la pamoja la Kijeshi lililokuwa likifanyika Mkoani Tanga lilifunguliwa rasmi tarehe 10 Febuari 2025 likishirikisha nchi kumi na Tano (15) ambazo ni Marekani, Ubeligiji, Comoro, Djibuti, Ufaransa, Georgia, Kenya, Madagascar, Malawi, Mauritius, Morocco, Msumbiji, Shelisheli, Somalia na Tanzania ambayo ni nchi mwenyeji.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.