Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litaadhimisha Siku ya Mashujaa kwa kutoa huduma za kijamii maeneo mbalimbali nchini kesho tarehe 25 Julai, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa JWTZ Kanali Ramadhani Dogoli amesema; Jeshi litatoa huduma ya vipimo bure kwa magonjwa yasioambukiza , kufanya usafi maeneo mbalimbali nchini pamoja na kutoa msaada wa kibinadamu katika vituo vya kulelea watoto yatima.
Aidha, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyoatatembelea wagonjwakatika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, kisha atakwenda kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja kujionea shughuli zinazoendelea na baadaye kuongea na Waandishi wa habari.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.