Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeadhimisha siku ya Mazingira duniani leo tarehe 05 Juni, 2021 kwa kufanya shughuli mbalimbali za utunzaji mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji miti, kufanya usafi namichezo.
Aidha, JWTZ limeadhimisha siku ya leo katika maeneo mbalimbali hapa nchini kama ifuatavyo:- Mkoani Tabora Maafisa na Askari wamefanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete, Mkoa wa Dar es Salaam wamefanya usafi katika Shule ya Msingi Changanyikeni, Hospitali ya Vijibweni, Hospitali ya Kigamboni na Barabara ya Tungi Ferry huko Kigamboni. Jijini Dodoma wamefanya usafi katika Soko la Ndugai, Hospitali ya Mkoa, na Hospitali ya Makole.
Vile vile, Maafisa na Askari wamefanya usafi katika Shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kijiji cha Pangawe Wilaya ya Morogoro Mjini. Pamoja na usafi wa mazingira, Maafisa na Askari hao wameshiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.