Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania leo tarehe 16 february 2018 limeungana na majeshi mengine duniani kuadhimisha siku ya michezo ya majeshi iliyofanyika katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Upanga jijini Dar es Salaam.
Siku ya michezo ya majeshi duniani (CISM) huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Februari lengo likiwa ni kueneza amani duniani kupitia michezo mbalimbali.
Hapo awali ilizoeleka kuwa majeshi hukutana wakati wa vita tu, hivyo baada ya vita kuu ya pili ya dunia Umoja wa Mataifa uliona iko haja ya kuwa na chombo ambacho kitawakutanisha wanajeshi wote kwenye michezo ili kudumisha amani, ndipo lilipozaliwa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM).
Baraza la Michezo la Majeshi Duniani lina jumla ya wanachama 132, na Tanzania ni moja ya nchi wanachama hai wa baraza hilo.
Maadhimisho ya siku ya michezo ya majeshi duniani imehudhuriwa na waambata jeshi wa nchi mbalimbali ikiwemo Uturuki, Nigeria, Kenya, Angola na Zimbabwe.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.