Hatimaye malori ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yameanza rasmi safari ya kuelekea mikoa ya Kusini na Pwani katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Joseph Pombe Magufuli la kusomba korosho na kuzipeleka katika maghala yaliyoteuliwa na Serikali.
Akizungumza na Madereva Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Meja Gaudence Ilonda amesema, JWTZ linaendelea na operesheni hiyo ambayo haitakuwa na athari yoyote kwa wananchi ambao wapo maeneo hayo kwa kuwa hii si Operesheni ya Kijeshi bali tunaenda kusaidia wananchi.
Aidha, Magari mengine yanaendelea kuondoka ili kutekeleza operesheni hiyo kwa weledi mkubwa na kwa muda muafaka, ambapo zaidi ya magari 70 yanategemewa kufika mikoa ya kusini na Pwani kwa ajili ya kusomba korosho kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Tawi la Uhandisi na Ugavi Brigedia Jenerali Paul Simuli amesema kuwa magari yapo ya kutosha ili kuhakikisha jukumu hilo linafanikiwa. Pamoja na hayo amewaasa madereva kufanyakazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni ili kuhakikisha operesheni inakamilika kwa wakati.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.