Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekabidhiwa Jengo la Chuo cha Ulinzi wa Taifa na Jeshi la Ukombozi la Jamhuri ya Watu wa China (PLA) lililojengwa Kunduchi Jijini Dar es Salaam kwa msaada wa Serikali ya nchi hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika Novemba 24, 2020.
JWTZ liliwakilishwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi na Matengenezo Jeshini, Kanali Hamza Mzee kutoka Makao Makuu ya Jeshi Dodoma na PLA iliwakilishwa na Msimamizi Mkuu wa Chuo hicho Brigedia Jenerali Zhu Dumei.
Aidha, awamu ya pili ya mradi huo ilianza rasmi tarehe 01 April, 2019 na kumalizika tarehe 25 Agosti, 2020, huu ukiwa ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na JWTZ kwa kudhaminiwa na Jeshi la Ukombozi la Jamhuri ya Watu wa China.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.