Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeonya vitendo vya utapeli vinavyofanywa na baadhi ya watu kuwarubuni vijana wanaotaka kujiunga na JWTZ kwa kupokea fedha zao.
Onyo hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ Luteni Kanali Gaudentius Ilonda alipokuwa anatoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari jijini Dar es salaam.
Kutokana na kadhia hiyo Luteni Kanali Ilonda aliwaomba wananchi kuwapuuza matapeli hao kwa kutokubali kudanganywa kwa kutoa fedha yoyote kwani JWTZ lina utaratibu wake wa kuandikisha vijana Jeshini.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.