Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi kwa wataalamu wa Tiba watakaotoa huduma za afya katika hospitali, vituo vya afya na zahanati za Jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, msemaji wa JWTZ Kanali Ramadhani Dogoli amesema, JWTZ limetoa nafasi ya kuandikishwa Jeshini kwa watanzania wenye taaluma zifuatazo:- Doctor of Medicine, Doctor of Dental Surgery, Bachelor of Pharmacy, BSC in Health System Management, Bachelor in Laboratory Science, Bachelor of Science in Nursing, Bachelor of Science in Physiotherapy na Bachelor of Science in Prosthetics and Orthotics.
Akifafanua zaidi Kanali Dogoli amesema, walengwa watakaoandikishwa Jeshini ni wale wenye sifa zifuatazo;-
a.Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa,
b.Awe na umri kati ya miaka 18 na 28,
c.Awe na afya njema ya mwili na akili,
d.Awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri na
e.Awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani na kufungwa jela
Pamoja na sifa hizo atakayependa kuandikishwa jeshini pia anatakiwa awe na;-
a. Cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate),
b.Vyeti vya shule (Academic & School Leaving Certificates) na
c.Vyeti vya Chuo (Transcript & Academic Certificates).
Aidha, Kanali Ramadhani Dogoli aliongeza kuwa, Daktari anatakiwa awe amemaliza mafunzo kwa vitendo (Internship) na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na Bodi. Vilevile anayehitaji anatakiwa awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.
Kanali Ramadhani Dogoli amewataka wenye sifa hizo na wanaohitaji kujiunga na JWTZ waripoti katika Kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo, Mgulani jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti 2018 kuanzia saa 1.00 Asubuhi kwa ajili ya usaili.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.