Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoaufafanuzi wa taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Jeshi limekata mazao na kubomoa makazi ya Wananchi wa maeneo ya Kisopwa, Mloganzila na Kiluvya “B” yaliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na Waandishi wa HabariMakao Makuu ya Jeshi hilo Upanga Jijin Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenziwa Habarina Uhusiano na Msemajiwa Jeshi hilo Luteni Kanali Gaudence Gervas Ilonda amesemakuwa eneohilo ni mali ya Jeshi na Wananchi waliovamia maeneo hayo waondoke ili kulipisha Jeshi hilo liendelee na Majukumu yake. Aidha, Luteni Kanali Illonda amesemakuwa sualahilo ni la muda mrefu na lilishapatiwa ufumbuzi kwa ngazi mbalimbali lakini wananchi hao wamekuwa wakikaidi Amri ya kuhama maeneo hayo.
Vile vileamewataka Wananchi nchini kote kuyaheshimu maeneo ya Jeshinakuziheshimu sheria za nchi. “Kwa mtu yeyote anaye fikiriakuvamia maeneo ya Jeshi aache mara moja kwani maeneo hayo si rafiki kwao na yametengwa kwaajili ya matumizi ya Jeshi na si vinginevyo” alisema Luteni Kanali Ilonda.
Hivyo basi Jeshi linawasihi Wananchi ambao watakuwa wananunua maeneo ambayo yako karibu na Kambi za Jeshi ni vema wakawasiliana na Jeshi hilo kabla yakununua maeneo hayo ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima baina ya Jeshi na Wananchi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.