Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania leo tarehe 02 Machi 2018 limewaaga Majenerali waliostaafu utumishi jeshini.
Sherehe za kuwaaga Majenerali hao zimefanyika katika Kambi ya Twalipo Mgulani Jijini Dar es Salaam huku zikiambatana na gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yao.
Majenerali walioagwa leo ni aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali James Mwakibolwa (Mstaafu), aliyekuwa Mkuu wa JKT Meja Jenerali Michael Isamuhyo (Mstaafu), Brigedia Jenerali Aaron Lukyaa (Mstaafu), Brigedia Jenerali Martine Kemwaga (Mstaafu), Brigedia Jenerali William Kivuyo (Mstaafu), Brigedia Jenerali Emmanuel Kapesa (Mstaafu), Brigedia Jenerali Francise Njau (Mstaafu) na Brigedia Jenerali Elizaphani Marembo (Mstaafu).
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.