Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeaga miili ya marehemu Koplo Marcelino Pascal Fubusa na Praiveti Venance Moses Chiboni, leo tarehe 16 Octoba 2017 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali James Mwakibolwa, Makamanda na Wanadhimu mbalimbali wa JWTZ pamoja na ndugu, jamaa na marafiki waliaga kwa huzuni miili ya marehemu hao.
Akizungumza wakati wa kuaga marehemu, Waziri wa Ulinzi na JKT amewataka maafisa na askari kutokata tamaa isipokuwa tukio hilo liwape nguvu na ushupavu katika kutekeleza majukumu yao.
Marehemu hao waliuawa wakiwa katika jukumu la Ulinzi wa Amani nchini DRC baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi tukio ambalo lilitokea tarehe 09 Octoba 2017 umbali wa kilomita 24 mashariki mwa mji wa Beni.
Baada ya tukio hilo la kushtukizwa, Majeshi yetu yalifanikiwa kuwarudisha nyuma waasi hao na kudhibiti eneo hilo.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.