Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, leo tarehe 24 Januari 2022 kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan amewavisha Nishani Maafisa na Askari wa JWTZ.
Zoezi hilo lililoongozwa na gwaride la Mapokezi kwa Mkuu wa Majeshi, limefanyika Ihumwa Jijini Dodoma ambapo Maafisa na Askari idadi 79 wamevishwa Nishani za Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Utumishi Uliotukuka, Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia njema.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.