Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)limekanusha taarifa zilizosambaa kwenyemitandao ya kijamiikuhusu mtoto aliyepatiwa matibabu ya kuvunjika mkono katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo. JWTZ limemtaka mlalamikaji afikishe taarifa hizo kwenye uongozi wa Jeshi hilo ili ikithibitika wahusika wachukuliwe hatua stahiki.
Akizungumza na vyombo vya habari, Msemaji wa JWTZ Kanali Ramadhani Dogoli amesema kuwa aliyepata tatizo kama hilo atoe taarifa kwa uongozi wa Jeshi ili asaidiwe.
Kwa upande wa Mkuu wa Tawi la Tiba Jeshini Meja Jenerali Denis Janga amesema JWTZ linajukumu la kuwalinda na kuwahudumia wananchi wakati wa amani na wakati wa vita. Aidha, hospitali zote za Jeshi ikiwemo Lugalo hutoa huduma stahiki kwa wananchi wote.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.