Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania leo tarehe 31 Julai 2022 limempokea rasmi bondia kutoka timu teule ya ngumi ya Jeshi Sajinitaji Sulemani Kidunda katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya kumaliza pambano lake la marudiano jana tarehe 30 Julai 2022 na bondia kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo Erick Tshimanga Kantompa na kuibuka na ushindi wa Mkanda WBF kwenye pambano hilo lililofanyika Mkoani Songea.
Aidha, Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Brigedia Jenerali Mbaraka Mkelemi alitoa pongezi zake kwa bondia wa JWTZ na kumtaka kuendeleza nidhamu katika mchezo huo na kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuliwakilisha Jeshi vema ndani na nje ya nchi.
Pia kwa mujibu wa bondia kutoka JWTZ Sajinitaji Sulemani Kidunda pambano la jana ni pambano lake la tisa tangu aanze kuingia ulingoni katika kuliwakilisha Jeshi kwenye mchezo wa ngumi. “Nidhamu ndio msingi mama katika mafanikio yangu tangu nianze mashindano ya ngumi” anasema Sulemani Kidunda.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.