Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imekabidhi trekta aina ya NEW HOLLAND lenye thamani ya shilingi milioni 48.37 kwa Kamandi ya Jeshi la Anga kwa ajili ya kufanyia usafi kwenye uwanja wa ndege wa jeshi uliopo Ngerengere. Makabidhiano hayo yalifanyika Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la JKT (SUMA JKT) Mlalakuwa jijini Dar es Salaam tarehe 07 Disemba 2020.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbuge alisema kwa upande wa JKT wao wameunga mkono jitihada hizo za kuiwezesha Kamandi kuhudumia vema kiwanja hicho kwa kununua mashine ya kufyekea iliyofungwa kwenye trekta hilo yenye thamani ya shilingi milion 8.5.
Nae mgeni rasmi Meja Jenerali Kaisy Njelekela aliyekuwa akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT, aliitaka Kamandi hiyo kulitunza trekta hilo ili liweze kutumika kwa muda mrefu.
Mwakilishi wa Kamandi hiyo Brigedia Jenerali Shaban Mani aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT kwa kuwapatia trekta hilo kwani litarahisisha shughuli ya utunzaji wa kiwanja cha ndege Ngerengere.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.