Kikundi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kinachoshiriki Ulinzi wa Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kimeshambuliwa kwa kushtukizwa na kundi la waasi la Siriri katika kijiji cha Dilapoko Kusini Magharibi mwa nchi hiyo tarehe 03 Juni, 2018.
Wakati wa shambulizi hilo Maafisa na Askari wa JWTZ walijibu mapigo kwa ujasiri na kufanikiwa kuwashinda nguvu waasi hao.
Aidha, mapambano hayo yalipelekea Askari mmoja wa JWTZ kupoteza maisha na wengine 18 kujeruhiwa.
Mipango ya kuurejesha nyumbani mwili wa Askari aliyeuawa inafanywa na Umoja wa Mataifa .
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.