Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo leo tarehe 26 Februari 2019 amefanya ziara Chato Mkoani Geita kwa kutembelea kisiwa cha Magafu kilichopo Ziwa Victoria na Uwanja wa Ndege wa Chato.
Ziara hiyo imefanyika kwa lengo la kujionea maeneo hayo ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa mipango endelevu ya Ulinzi katika maeneo yanayoizunguka Ziwa Victoria.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Majeshi aliongozana na Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Meja Jenerali George Ingram na Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Meja Jenerali Richard Makanzo
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.