Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimefanyika tarehe 26 Aprili 2017 mjini Dodoma mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Ni sherehe ambayo huadhimishwa kila mwaka nchini kwa kuzaliwa Tanzania. Ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania sikukuu hii kufanyika kitaifa mjini Dodoma.
Sherehe hizo zilipambwa kwa maonesho mbalimbali ikiwepo gwaride maalum lililoandaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama, maonesho ya mbwa bila kusahau utimamu wa mwili uliooneshwa na makomandoo wa JWTZ ukiwavutia wengi katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.