Sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yamefanyika Januari 12, 2020 katika Uwanja wa Aman, Zanzibar.
Maadhimisho hayo yaliongozwa na Rais na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakiwemo wastaafu.
Baadhi ya viongozi hao ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Wengine ni Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Aman Abeid Karume.
Akihutubia wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo, Rais Dkt. Shein alisema Serikali anayoiongoza itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kikatiba na kisheria katika kulinda amani, utulivu na maisha ya wananchi na mali zao.
Aliendelea kusema kuwa suala la kudumisha amani halina mbadala na kusisitiza kuwa Serikali haitosita kumchukulia hatua mtu yeyote atakaejaribu kuhatarisha amani ya nchi.
Aidha, Maadhimisho hayo yalipambwa na vitendo vya kijasiri vilivyoonyeshwa na makomando kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania .
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.