Mafunzo ya Makocha wa mchezo wa Ngumi na Mpira wa Kikapu yaliyokuwa yakiendeshwa kwa Makocha wa JWTZ yamefungwa rasmi tarehe 01 Februari 2018 kwenye Kambi ya JKT Mgulani.
Mafunzo hayo yalijumuisha Makocha wa michezo hiyo kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo JWTZ, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na wengine kutoka Taasisi mbalimbali.
Akifunga mafunzo hayo mgeni rasmi Brigedia Jenerali Suleimani Mzee amewataka wahitimu hao kwenda kukifanyia kazi kile ambacho wamejifunza katika kipindi chote cha wiki mbili ili kuweza kuibua na kukuza vipaji vya Wanamichezo wetu.
Naye Mkufunzi kutoka Ujerumani Kapteni Paul Klar ameushukuru uongozi wa Jeshi na Washiriki kwa kuonesha ushirikiano wa karibu kwa kipindi chote cha mafunzo na kusema wana imani mafunzo hayo yatazaa matunda mema.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wahitimu wenzake mwakilishi wa wahitimu hao Meja Kelvin Byabato ameushukuru uongozi wa Jeshi kupitia Ubalozi wa Tanzania na Mwakilishi wa Jeshi katika Baraza la Michezo ya Kijeshi Duniani (CISM),Kanali Joseph Bakar, kuwa kitendo cha kuwaleta wakufunzi hao kitawaongezea ujuzi na mbinu mpya katika michezo hiyo na hivyo kuzifanya timu za Jeshi na ya Taifa kuwa na watu wenye sifa na kuliletea sifa Taifa letu.
Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 22 Oktoba 2018 na kufungwa tarehe 01 Novemba 2018.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.