Ama kweli Kutangulia siyo kufika na Riziki ya Mja haipotei bali huja kwa wakati autakao Mola, kauli hizi zilijidhihirisha pale Mwanariadha wa TanzaniaMagdalena Crispin Shauri alipowashangaza wengi na kutoamini kile kilichokuwa kikitokea kwa watu waliofurika kushuhudia Mbio za Nyika (10 Km) katika Viwanja vya Kambi ya Jeshi la Nchi Kavu(Kahawa Barracks) hapa Nairobi nchini Kenya alipotoka nyuma na kumpita Mkenya Perine Nenkampi aliyekuwa akiongoza mbio hizo na kufanikiwa kumpita meta10 kabla ya kumaliza mbio hizo
Kitendo hicho kiliibua shangwe siyo tu kwa Watanzania bali hata kwa wale ambao waliokuwa wakifuatilia mpambano huo mkali baina ya wawili hao. .
Katika mchezo huo uliogawanyika katika makundi mawili yaani Wanaume na Wanawake Magdalena Crispin Shauri aliyemaliza nafasi ya kwanza kwa kutumia 33:09:22, na kupata medali ya Dhahabu, akifuatiwa na Mkenya Perine Nenkampi 33:12:07 (Silver) na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Doreen Chesang waKenya 33:23:02 aliyepata Bronze
Kwa upande wa Wanaume, Mkenya Kibinot Kandie alishika nafasi ya Kwanza kwa kutumia 28:42:05 alipata Medali ya Dhahabu huku akifuatiwa na Mkenya Phenus Kipleting aliyetumia 28:49:02, nafasi ya tatu ilichukuliwa na Isaac Kibet kutoka Uganda kwa kutumia 28:55:00.
Mchezo huo ulianza majira ya saa Tatu asubuhi na kufunguliwa rasmi na Makamu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Kenya Luteni Jenerali Robert Kibochi uliwavutia watu wengi.
Viongozi mbalimbali wa Majeshi na wengine kutoka katika Jumuiya Afrika Mashariki walihudhiria wakati wa Mchezo huo. Miongoni wa wageni hao ni Makamu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Burundi Meja Jenerali Joseph Ndayishimiye,Mkuu wa Msafara wa Tanzania Meja Jenerali Othman Sharif, Mwenyekiti wa Maandalizi ya Michezo ya Majeshi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki Meja Jenerali Ferdinand Safari, Mkuu wa Msafara wa Uganda Brigedia Jenerali Francis Takirwa, Mkuu wa Msafara wa Rwanda Brigedia Jenerali Emmanuel Bayinganana Mkuu wa Msafara wa Burundi Kanali Jean Habarugira na wengine.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.