Mahafali ya 38 ya Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) yamefanyika leo tarehe 15 Julai 2024, Duluti Arusha.
Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomina Tax akiambatana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Salum Othmani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo hicho pamoja na viongozi mbalimbali wa juu wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Chuo hicho Brigedia Jenerali Stephen Mnkande amesema jumla ya Maafisa wanafunzi 69 wamehitimu kozi leo ambapo 45 ni kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na 24 kutoka Majeshi rafiki ya Mataifa mbalimbali barani Afrika.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.