Mhe. Balozi Seif Ali Idd ambae alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo aliambatana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dk Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo.
Katika sherehe hizo wahitimu wapatao thelathini na nne walifanikiwa kuhitimu kozi zao katika ngazi ya Shahada ya uzamili na stashahada na kutunikiwa vyeti vyao.
Mhe. Balozi Seif Ali Idd aliwaasa wahitimu hao kutumia maarifa waliyoyapata kwa ufanisi ili kuleta ubora wa kazi wenye tija kwa manufaa ya nchi zao.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.