Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amelipongeza Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa CISM.
Daktari Mpango aliwasisitiza wajumbe kuwa Baraza hilo lipo katika kujenga amani na upendo miongoni mwa nchi wanachama ambapo alihimiza CISM kuendelea kuhubiri Amani na Upendo kupitia michezo.
Naye, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax amesema Mkutano huu wa 79 unawakutanisha wanachama, kubadilishana uwezo na kujenga maelewano kupitia michezo.
Amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda Kwa maandalizi na kufanyika kwa mkutano huo wa kihistoria.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amesema mkutano mkuu wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani nchini kunaleta tija na fursa mbalimbali kutokana na uwepo wa washiriki kutoka nchi hizo.
Mkutano wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) unafanyika nchini ikiwa ni mara ya pili, baada ya mwaka 1991 mwezi Mei Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa CISM uliofanyika Jijini Arusha.
Wajumbe wa mkutano huo watafanya ziara kutembelea sehemu mbalimbali za vivutio vya utalii Jijini Dar es Salaam na Zanzibar ili kuitangaza Tanzania.
Mkutano mkuu wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani umefunguliwa rasmi leo tarehe 14 Mei 2024 na utamalizika tarehe 19 Mei 2023.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.