Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo amewaongoza maelfu ya waombolezaji katika kutoa Heshima za Mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Shughuli hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, kidini, vyama za kisiasa na wananchi, ambapo Waziri Mkuu alipata fursa ya kutoa hotuba fupi ya salamu za rambirambi kwa wananchi.
Mbali na Uwanja wa CCM Kirumba wenye uwezo wa kuketisha watu 30,000 kufurika, mitaa na barabara zinazounganisha Jiji la Mwanza na Miji ya Sengerema, Geita hadi Chato ilipambwa na Mamia ya Maelfu ya Wakazi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa waliojitokeza kumuaga Mpendwa wao.
Mwili wa Kipenzi cha Watanzania, Hayati Dkt. John Magufuli umefikishwa hadi nyumbani kwake Chato, mkoani Geita ambapo wananchi watapata fursa ya kutoa Heshima zao za mwisho kesho 25 Machi 2021.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.