Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda amefunga rasmi mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi la mchezo wa Gofu "CDF Golf Trophy 2022" katika viwanja vya Gofu Lugalo Jijini Dar es Salaam na kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa mchezo huo.
Mashindano hayo yalihusisha vilabu mbalimbali vya mchezo wa Gofu hapa nchini pamoja na Klabu ya Gofu kutoka Lilongwe nchini Malawi ikiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Malawi Jenerali Vincent Nundwe aliyeambatana na Maafisa Jenerali kutoka nchini humo.
Awali ya yote Mwenyekiti wa klabu ya mchezo wa Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Michael Luhongo (Mstaafu) alimkaribisha mgeni maalum Mkuu wa Majeshi ya Malawi Jenerali Vincent Nundwe ambaye alitoa zawadi kwa Jenerali Jacob Mkunda na kumpongeza Kwa kuteuliwa kwake kuwa mlezi mpya wa Klabu ya Gofu Lugalo, nafasi ambayo alikabidhiwa na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu),
Jenerali Nundwe pia alipata fursa ya kutoa zawadi kwa Jenerali George Waitara (mstaafu), Meja Jenerali Said Mkambi na Brigedia Jenerali Michael Luhongo (mstaafu) kwa kuuendeleza na kujenga hamasa ya mchezo huo ambapo alisema kuwa mchezo wa gofu unajenga umoja na kuimarisha undugu kitaifa na kimataifa.
Jenerali Nundwe ameialika Klabu ya mchezo wa gofu Lugalo kwenda nchini Malawi mwezi Novemba mwaka huu kwa ajili ya kushiriki mchezo wa golf nchini humo.
Sambamba na hilo mwakilishi wa Benki ya NMB ndugu Philbert Mponzi alimshukuru Jenerali Mkunda kwa kuendeleza mchezo wa Golf na kuahidi kuwa Benki ya NMB itaendelea kuwa miongoni mwa wadhamini wa mchezo huo.
Jenerali Jacob Mkunda alihitimisha shughuli hiyo kwa kumshukuru Mkuu wa Majeshi ya Malawi Jenerali Vincent Nundwe, Maafisa na Wadhamini, Wachezaji na Wadau wa mchezo huo kwa kuboresha na kuuendeleza klabu ya mchezo wa gofu LugaloTanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.