Tarehe 13 Agosti Mwaka huu Waziri wa Ulinzi wa Kenya Balozi Raychelle Omamo alifungua rasmi Mashindano ya Majeshi kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Moi International Sports Center Kasarani ambapo jumla ya nchi Sita za Jumuiya hiyo zinashiriki mashindano hayo ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudani ya Kusini.
Mashinadano hayo yanajumuisha michezo mitano ambayo ni Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu na Riadha.
Tanzania inajumla ya Timu tano katika Mashindano hayo ambazo ni timu ya Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu na Riadha.
Katika ufunguzi wa Mashindano hayo mwenye Kenya inayowakilishwa na Timu ya “Ulinzi Stars” alifungua dimba kwa mchezo wa Mpira wa Miguu wakiikaribisha timu ya Jeshi la Burundi Muzinga FC. Katika mchezo huo wa ufunguzi Ulinzi iliweza kuibuka na ushindi wa mabao manne kwa bila (4-0).
Aidha, Waziri Balozi Omamo aliwataka wachezaji wanaocheza michezo mbalimbali katika mashindano hayo watambue kuwa lengo la mashindano hayo nu kuendelea kuiimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa katika masuala mazima ya Amani na auatulivu kwa nchi wanachama kupitia michezo.
Mashindano hayo yaliendelea tena leo tarehe 14 Agosti 2019 kwa kuzikutanisha nchi za Tanzania na Rwanda katika mchezo wa Mpira wa Peta na Tanzania kuweza kuibuka na ushindi mnono wa magoli 66-16. Katika mchezo huo mchezaji wa TanzaniaKoplo Mwanaidi aliweza kuibunka mfungaji bora kwa kufunga jumla ya magoli 55 kati ya 66 yalifungwa na timu ya Tanzania dhidi ya Rwanda. Uganda iliifundga Burundi 114-09.
Michezo mingine iliyochezwa leo ni pamoja na Mpira wa Miguu kati ya Rwanda dhidi ya Uganda na mpaka mwishi wa mchezo huo Rwanda (ARP FC) iliibuka na ushindi wa 1-0.
Kwa upande Mpira wa Kikapu Tanzania iliangukia pua kwa kupoteza mchezo huo kwa tofauti ya magoli manne dhidi ya Burundi yaani 79-75. Michezo mingine ni kati ya Rwanda na Uganda, ambapo Rwanda imeshinda 71-64, mchezo kati ya mwenyeji Kenya na Sudan Kusini ambapo mpaka sasa mwenyeji anaongoza kwa vikapu 26-22 lakini mchezo bado unaendelea.
VilevileMpira wa Wavu leo ulizikutanisha timu za Tanzania na Rwanda na Rwanda kuibuka mshindi kwa kushinda awamu zote tatu za mchezo kwa 25-21, 25-15 na 20-16. Mashindano hayo yataendelea tena kesho kwa Tanzania kushuka dimbani kupambana na Burundi kwenye mchezo wa Mpira wa Miguu.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.