• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe afungua rasmi mashindano ya kombe la Mkuu wa Majeshi

Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe afungua rasmi mashindano ya kombe la Mkuu wa Majeshi Posted On: Monday, 29th May 2017

Mashindano haya yalianzishwa rasmi mwaka 2014. Lengo la mashindano haya ni kudumisha mshikamano, kuvumbua na kukuza vipaji, pia mashindano hayo yatatumika katika kuteua kombaini ya timu ya JWTZ itakayowakilisha Jeshi na Taifa kwa ujumla katika mashindano ya michezo ya Majeshi na utamaduni kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo mwaka huu 2017, yanatarajiwa kufanyika nchini Burundi baadaye mwezi wa nane.

Kauli Mbiu ya mashindano haya ni, “Tushiriki Michezo kama sehemu ya Kazi, Kulinda Afya zetu na kudumisha mshikamano”. Michezo ni furaha na zaidi michezo inakuza nidhamu pamoja na kujenga afya ya mwili na akili kwa Wanajeshi.

Timu zinazoshiriki mashindano haya ni Ngome (Makao Makuu JWTZ), Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu, Kamandi ya Jeshi la Anga, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT).

Mashindano haya yanahusisha michezo ifuatayo; Mpira wa miguu kwa Wanaume, Mpira wa kikapu kwa Wanaume, Mpira wa mikono kwa Wanaume, Mpira wa pete kwa Wanawake, Mpira wa wavu kwa Wanawake na Mbio za nyika kwa Wanaume na Wanawake. Michezo hii inafanyika katika Viwanja vya Twalipo vilivyopo Mgulani pamoja na Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Mwaka huu mashindano haya yamefunguliwa rasmi tarehe 26 Mei 2017, katika Uwanja wa Uhuru na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb),. Aidha, Mashindano haya yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 06 Juni 2017.

Habari Mpya

  • Mkutano wa Wakuu wa Rasilimali Watu wa Jeshi wa Nchi za Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

    Mkutano wa Wakuu wa Rasilimali Watu wa Jeshi wa Nchi za Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

    tokea wiki 2
  • Zoezi KAA TAYARI lafungwa

    Zoezi KAA TAYARI lafungwa

    tokea wiki 2
  • Mnadhimu Mkuu JWTZ Afungua Kikao cha Wakuu wa Tiba kwa Majeshi nchi za SADC

    Mnadhimu Mkuu JWTZ Afungua Kikao cha Wakuu wa Tiba kwa Majeshi nchi za SADC

    tokea mwezi 1
  • NAFASI ZA KUJIUNGA NA JESHI

    NAFASI ZA KUJIUNGA NA JESHI

    tokea miezi 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 6
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 6
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 6
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miezi 8
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.