Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amekabidhi mabasi makubwa idadi tatu kwa JWTZ na basi moja dogo kwa Jeshi la Magereza baada ya magari hayo kufanyiwa ukarabati na kampuni ya Dar Coach Ltd iliyopo jijini Dar es Salaam.
Hafla ya makabidhiano imefanyika leo katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vilivyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Aidha, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) LuteniJenerali Yakubu Mohamed amemshukuru Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Makonda kwa kuvisaidia Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kutatua changamoto za usafiri.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.