Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salim Haji Othman ameyataka majeshi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuimarisha ulinzi katika kupambana na ugaidi ndani ya nchi zao.
Hayo yamesemwa kwa niaba yake na Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi Meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona alipokuwa akifungua Mkutano wa Wakuu wa Rasilimali Watu wa Jeshi wa Nchi za Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Mkutano huo unafanyika kisiwani Unguja Zanzibar.Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.