Mkuu wa Kamandi ya Vikosi Chini ya Makao Makuu ya Jeshi Meja Jenerali Iddi Nkambi kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi John Mkunda amekutana na Kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Akiba Kutoka Nchini Uganda Meja Jenerali Willium Don Nabasa pamoja na timu yake katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi ya zamani yaliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo Meja Jenerali Nkambi amesema Tanzania na Uganda ni nchi zenye historia kubwa katika masuala mbalimbali ya ushirikiano toka enzi za uongozi wa Hayati Mwalimu Nyerere, hivyo kuja kwao nchini ni sehemu moja wapo ya kujifunza masuala mbalimbali ya utendaji ndani ya Jeshi la akiba pamoja na kuendelea kushirikiana kutatua changamoto mbalimbali za kiutendeji kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuweza kupiga hatua zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Akiba kutoka nchini Uganda Meja Jenerali Nabasa, amelishukuru Jeshi la wananchi wa Tanzania pamoja na serikali kwa ujumla kwa kuendelea kushirikiana nao huku akisema wamekuja nchini kwa lengo la Kujifunza masuala mbalimbali ya utendaji yanayohusu Jeshi la Akiba.
Mkuu huyo wa Jeshi la akiba pamoja na timu yake kutoka nchini Uganda wapo nchini kwa ziara maalumu kwa lengo la kuona, kujifunza na kujadiliana na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la akiba nchini Brigedia Jenerali Erick Mlelwa masuala mbalimbali yanayohusiana na Jeshi la akiba nchini.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.