Mkuu wa jeshi la Lesotho, luteni Jenerali Tlali Kamoli na ujumbe wake, ametembelea Makao Makuu ya Jeshi ikiwa ni jitihada ya kudumisha uhusiano kati ya nchi mbili hizi. Katika ziara hiyo, Luteni Jenerali Kamoli, alikutana na mwenyeji wake Jenerali Davis mwamunyange, na kuzungumzia ushirikiano kijeshi, Jenerali Kamoli alipokea zawadi ya nembo ya JWTZ kutoka kwa mwenyeji wake, na kushukuru uongozi wa jeshi kwa ukarimu waliouonyesha.
Mkuu huyo wa majeshi wa Lesotho alipata fursa ya kutembelea SUMA JKT kuangalia mradi wa matrekta, na kusifu jitihada za JKT katika kuchochea maendeleo ya kilimo nchini.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.