Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda tarehe 05 Julai 2022 amekabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa mtangulizi wake Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ambaye amestaafu utumishi jeshini.
Jenerali Mkunda aliwasili Makao Makuu ya Jeshi (MMJ) muda wa saa mbili na nusu asuhuhi (0830) Jijini Dodoma na kukagua gwaride Maalum iliyoandaliwa kwa ajili yake ikiwa ndio mara ya kwanza kufika Makao Makuu ya JWTZ akiwaMkuu wa Majeshi na kisha kusalimiana na Makamanda na Wanadhimu wa JWTZ wakiongozwa na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Haji Othman.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Mkunda aliapishwa tarehe30 Juni 2022 baada ya kuteuliwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo kufuatia aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venus Mabeyo kustaafu kwa heshima kwa umri.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.