Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo amewavisha vyeo Maafisa Wakuu waliopandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 12 Aprili, 2018.
Tukio hilo la uvishaji vyeo limefanyika leo tarehe 16 Aprili, 2018 Makao Makuu ya Jeshi, Upanga Jijini DSM. Maafisa Wakuu waliovishwa vyeo ni kwa vyeo vya Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali, Brigedia Jenerali kuwa Meja Jenerali,Kanali kuwa Brigedia Jenerali na Luteni Kanali kuwa Kanali
Aidha, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi amewapongeza Maafisa Wakuu hao na kuwatakia kila la kheri katika vyeo vyao vipya.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.