Mkuu wa Majeshi wa Uganda Jenerali Wilson Mbadi hivi karibuni aliwasili nchini kwa ziara ya kikazi na kupokelewa kwa gwaride maalumu katika Viwanja vya ofisi ndogo ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kupokelewa alifanya mazungumzo na mwenyeji wake Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Mathew Mkingule, Wakuu wa Kamandi na Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi. Lengo la mazungumzo ni kuimarisha Ushirikiano baina ya majeshi ya nchi hizi mbili.
Aidha, alipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt . Stergomena Lawrence Tax (mb) pamoja na kutembelea Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) kilichopo Kunduchi Dar es Salaam na maeneo mbalimbali Kisiwani Zanzibar.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.