Mkuu wa Majeshi ya Msumbiji Admiral Joaquin Rivas Mangrasse amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda wakati wa ziara yake ya kikazi hapa nchini.
Mara baada ya kuwasili, Mkuu wa Majeshi ya Msumbiji alikagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Aidha, Mkuu huyo wa Majeshi alipata fursa ya kusalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax.
Ziara hiyo inalenga kuongeza ushirikiano wa kijeshi baina ya Tanzania na Msumbiji ili kuboresha na kuimarisha ulinzi na usalama baina ya nchi hizi mbili.
Katika mazungumzo yao wakuu hao wa Majeshi wamesema usalama wa nchi hizi utachangia maendeleo ya wananchi wake.
Ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji umedumu kwa muda mrefu tangu enzi za waasisi wa mataifa haya Hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Samora Machel wa Msumbiji.Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.