Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) pamoja na Luteni Jenerali Salim Haji Othman kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
Kabla ya kiapo hicho cha utii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu aliwavalisha vyeo vipya Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na Meja Jenerali Salim Haji Othman kuwa Luteni Jenerali.
Mara baada ya kuapishwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Stergomena Tax aliwapongeza na kusema hana mashaka na utendaji kazi wao.
Kwa upande wake Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mhe Samia Suluhu Hassan amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kwa utendaji wake na kuahidi kuendelea kumtumia kwenye majukumu mbalimbali atakazompangia
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.