Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo leo Octoba 9 amefanya ziara kutembelea ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge Railway) unaoendelea nchini. Reli hiyo inaanzia Dar es salaam hadi Dodoma.
Jenerali Mabeyo alitembelea ujenzi huo na kujionea hali halisi inavyoendelea ambapo alianza kwa kufika Makao Makuu ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Mkurungenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Masanja Kadogosa, na kisha kupata maelezo mafupi kutoka kwa msimamizi mkuu wa mradi huo.
Ziara hiyo ilianza kwa kutembelea eneo la Kamata ambalo ujenzi wa daraja la treni litakalopita juu unaendelea ili kuepusha muingiliano kati ya barabara na reli.
Jenerali Mabeyo alihitimisha ziara yake katika maeneo ya Mkoa wa Pwani, pia alisifia mradi huo kuwa ni miongoni mwa miradi ya kisasa zaidi Barani Afrika na katika Ukanda wetu wa nchi za Afrika Mashariki. Aidha, alisema kwa upande wa Jeshi, reli hiyo itasaidia kusafirisha vifaa na mizingo mbalimbali ya kijeshi na kuihakikishia Serikali kuwa Jeshi itailinda reli hiyo kwa maslahi ya Taifa.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.