Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewavisha nishani Maafisa na Askari wa Vikosi vilivyoko Kanda ya Dar es salaam na Pwani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan.
Zoezi hilo limefanyika Jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa Mgulani tarehe 7 Juni 2024 kwa kuwavisha Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, Nishani ya Utumishi Mrefu na Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia njema.
Wakati huo huo, Jenerali Mkunda amewavisha Nishani ya Ulinzi wa Amani ya SADC Maafisa na Askari kwa niaba ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kwa kutambua mchango wao katika Ulinzi wa Amani nchini Msumbiji chini ya Mwanvuli wa SADC iliyowatunuku Nishani hiyo.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.