Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi Jenerali Vincent Nundwe leo tarehe 24 Agosti 2022 amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi ya zamani yaliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Jacob Mkunda.
Katika mazungumzo yao, Jenerali Nundwe amesisitiza ushirikiano uliopo baina ya Jeshi la Malawi na Tanzania uendelee kudumishwa na ikiwezekana yaangaliwe maeneo mengine ambayo majeshi haya yanaweza kuongeza wigo wa ushirikiano.
Pia, Jenerali Nundwe amempongeza Jenerali Mkunda kwa kuteuliwa kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, na akamuahidi kumpa ushirikiano wakati wowote atakapohitajika.
Naye Jenerali Mkunda amemshukuru mgeni wake kwa kufanya ziara ya kikazi nchini, na akamuahidi ushirikiano uliopo utaendelea kudumishwa ili uendelee kuleta manufaa kwa majeshi yote mawili.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.