Mkuu wa Utumishi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali Blasius Masanja leo Julai 28,2018 amefunga rasmi mafunzo ya kuruti kundi maalumu la pili, sherehe hiyo iliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya awali ya kijeshi RTS Kihangaiko kilichopo Msata wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Aidha Meja Jenerali Masanja aliwataka askari hao waliohitimu mafunzo yao ya awali kutii kiapo chao na watambue kuwa jukumu kubwa lililo mbele yao ni kulinda amani ya nchi na mipaka yake na vilevile wawe tayari kufanya kazi mahala popote ndani na nje ya nchi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.