Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman leo tarehe 26 Februari amefunga Kikao cha Wakuu wa Viwanda na Mashirika ya Kijeshi ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Hoteli ya Twiga iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo Luteni Jenerali Othman amesisitiza umuhimu wa kuwa na umoja na ushirikiano baina ya wanajumuiya hasa katika nyanja za kiteknolojia ili kukuza viwanda vya nchi wanachama, kuleta ushindani kimataifa na hatimae kukuza uchumi wa jumuiya hiyo kwa ujumla.
Aidha, amesisitiza kuyatilia mkazo makubaliano yaliyofikiwa na pia kutatua changamoto ambazo bado hazijatatuliwa na kuziweka sawa kwa manufaa ya Jumuiya nzima.
Ufungaji wa kikao hicho umehudhuriwa na wajumbe kutoka nchi ya Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda, Sudani ya Kusini na Somalia ambapo Tanzania ilikuwa mwenyeji wa kikao hicho.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.