Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Mathew Mkingule leo tarehe 23 Mei 2022 amefungua Semina ya Wataalamu wa Saikolojia na Masuala ya Jamii iliyoandaliwa na JWTZ. Semina hiyo imehudhuriwa na Wataalamu wa Saikolojia kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini iliyofanyika Jenerali Mabeyo Complex - Mabele hall, jijini Dodoma.
Akizungumza katika semina hiyo Luteni Jenerali Mkingule amewataka wajumbe wa Semina hiyo kutafuta njia za kukabiliana na changamoto zinazotokana na afya ya akili kwa Maafisa na Askari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Aidha, Mkurugenzi wa Masuala ya Jamii Jeshini Brigedia Jenerali Solotina Nshushi amewataka wataalamu hao kuhakikisha wanamaliza changamoto za Kijamii za Maafisa na Askari waliopo kwenye vyombo vyao.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.